ZUHURA SHABAN KAMA NI RAHISI lyrics

KAMA NI RAHISI

ZUHURA SHABAN

GENRE
R&B
KAMA NI RAHISI

Kama ni rahisi ungelianza ili kuyatenda
Sina wasiwasi wakuyapoteza niliyoyaunda
Natoa nafasi kwa anayeweza aje kunishinda
Ameshanihisi kwake napendeza ndiyo kanipenda

Aliponitaka ili niwe wake sikumhofia
Sikuwa na shaka hilo ombi lake nimelipokea
Sikubabaika tangu anitake nimeshatulia
Sitobadilika naipata kwake raha ya dunia

Kama ni rahisi ungelianza Ili kuyatenda
Sina wasiwasi wakuyapoteza niliyoyaunda
Natoa nafasi kwa anayeweza aje kunishinda
Ameshanihisi kwake napendeza ndiyo kanipenda

Mapenzi adhimu yasiyo mithali yameniingia
Tena ni matamu kuliko asali nayafurahia
Walonilaumu potelea mbali leo nawaambia
Sitojidhulumu kwa wangu mpenzi nikaangaamia

Kama ni rahisi ungelianza ili kuyatenda
Sina wasiwasi wakuyapoteza niliyoyaunda
Natoa nafasi kwa anayeweza ajе kunishinda
Ameshanihisi kwake napendеza ndiyo kanipenda

Nimemuamini ni wangu mlezi anayenileya
Wangu wa moyoni tena namuenzi namnyenyekea
Nakula yamini pendo sigeuzi nimeswafi nia
Uovu asilini kwa wangu mpenzi sitomtendea

Kama ni rahisi ungelianza ili kuyatenda
Sina wasiwasi wakuyapoteza niliyoyaunda
Natoa nafasi kwa anayeweza aje kunishinda
Ameshanihisi kwake napendeza ndiyo kanipenda

Toka awe wangu nami niwe wake kigiuu na njia
Mara mje kwangu mara mwende kwake fitina kutia
Hili pendo langu kwake liondoke mmedhamiria
Yabaki machungu kisha mtucheke na kuhadithia

Kama ni rahisi ungelianza ili kuyatenda
Sina wasiwasi wakuyapoteza niliyoyaunda
Natoa nafasi kwa anayeweza aje kunishinda
Ameshanihisi kwake napendeza ndiyo kanipenda

Mtafanya nini, mtafanya nini?
Pendo letu la wawili nyie lawaudhi nini nyie?

Mtafanya nini, mtafanya nini?
Penzi letu la wawili linawaudhi nini nyie?

Umbea unakazi eleweni mafitina
Kazi yenu uchochezi
Lengo lenu tuachane

Si mikiki si biriti lilomlewesha bwana nyie

Mtafanya nini, mtafanya nini?
Penzi letu la wawili nyie lawaudhi nini nyie?

Kama munadhani ni rahisi mungeanza kuyaunnda
Mimi sina wasiwasi najiamini napendwa
Naye kwangu kajihisi ndomana ameniganda mimi

Mtafanya nini, mtafanya nini?
Huba zetu za halali zinawakata maini
Mumeona twapendana roho zinakuumeni
Wapenzi tumeshibana hatujali mafitini
Pendo letu limefaana linawakata maini nyie

Mtafanya nini, mtafanya nini?
Hamuezi kutuzidi tushakolea pendoni sie
Mtafanya nini, mtafanya nini?
Pendo letu la wawili nyie lawaudhi nini nyie?
©Shariff Kombo +254 743 144 211

Related songs

ChampionsQuest DivaMAS Maxwell47Shawnn Love OnlineCoupdekat GRIMY FREESTYLEKIDx Lawrence Takes OverGo-Kart Mozart Square 1FLORESMUSIC LA DREAMSSHAWN E Got It Like ThatB.I From the Back of a CabRostam

Comments

Popular posts from this blog